19 Aprili 2015 - 11:29
Mapigano yanaendelea Yemen, Mashia wazidi kusonga mbele

Wakati huo huo ndege za Marekani zisizo na rubani zimeendelea kuwasaidia magaidi wanaomuunga mkono rais Hadi kupambana na majeshi ya wanamapinduzi wa kishia wa Huthi.

Mapigano kati ya wanamapinduzi wa kishia wa Huthi na vikosi vinavyomuunga mkono rais Abedrabbo Mansur Hadi yameendelea jana usiku kusini ya Yemen na kusababisha vifo ya watu 21 huku hujuma za ndege za kivita za nchi shirika zinazoongozwa na Saud Arabia na Marekani zikiendelea kuangusha mabomu katika makazi ya raia wa Yemen kwa wiki ya nne hivi sasa.

Saudia arabia imekuwa ikishambulia makazi ya wananchi, shule, wizara za nchi na hata mahospitali.

Wanaharakati wa kishia wa Huthi 10 wafuasi wanne wa  serikali na "kamati za umma" na wananchi kadhaa wasio na hatia wanaripotiwa kuuawa katika mashambulizi hayo ya Saudia arabia.

Zaidi ya Wanamgambo 20 wa makundi ya kigaidi  wanaomuunga mkono rais Rais Hadi aliyekimbilia Saud Arabia wameuwawa katika mapigano ya leo alfajiri katika mji wa kusini magharibi wa Taez. Wanamapinduzi wa kishia wa kabila la Huthi wanasemekana kutuma wapiganaji zaidi katika mji wa  Taez kutoka miji ya Hodeida na Ibb.

Wakati huo huo ndege za Marekani zisizo na rubani zimeendelea kuwasaidia magaidi wanaomuunga mkono rais Hadi kupambana na majeshi ya wanamapinduzi wa kishia wa Huthi.